- AdelPhil Online Academy
- Posts
- AdelPhil Online Academy imehamia hapa
AdelPhil Online Academy imehamia hapa
AdelPhil Online Academy, moja ya vyuo vya kwanza Tanzania vya elimu ya mtandaoni, sasa inahamia hapa kutoka makazi yake ya sasa hapa.
AdelPhil Online Academy ni taasisi ya elimu mtandaoni inayolenga
Kukupatia uelewa mpya
Kukuongezea/kuboresha uelewa ulionao.
AdelPhil Online Academy inatumia teknolojia ya kisasa kabisa katika utoaji wa elimu.
Kinyume na mfumo wa elimu uliozoeleka wa "kutoka juu kwenda chini" ambapo maamuzi yote kuhusu elimu kwa mwanafunzi hufanywa na taasisi na/au mwalimu, AdelPhil Online Academy inampa mwanafunzi uwezo wa kushiriki maamuzi yanayohusu kozi/masomo husika.
Karibu sana kushiriki katika mapinduzi haya ya sekta ya elimu.
Kozi za awali zitakuwa
Usalama wa mtandaoni (Cybersecurity)
Jinsi ya kuwa mtu bora (personal development)
Stoicism
Maelezo zaidi yatawajia hapa.
Asanteni na karibuni.
Reply