#JinsiYaKuwaMtuBora: kila tunakopita, msisitizo ni kwamba tuwe watu wema kwa wenzetu. Lakini huwezi kuwa mwema kwa mtu mwingine bila kuwa mtu mwema kwako mwenyewe pia
Kwa tuliopata malezi mazuri, jambo moja tulilokuwa tunasisitizwa tangu utotoni ni kuwa wema kwa wenzetu. Kwa Wakristo kama kocha wako, kuna mistari kwenye Biblia Takatifu inayosisitiza kuhusu hilo.
Na hakuna tatizo kuwa mtu mwema kwa wenzetu. Na kwa hakika dunia ingekuwa mahala pazuri sana kuishi endapo sote tungezingatia umuhimu wa kuwa wema kwa wenzet…