Kozi ya Wiki Nane ya TAHAJUDI (meditation): Wiki ya Kwanza - Jinsi ya Kudhibiti Stress
Karibu katika kozi hii ya wiki nane ya TAHAJUDI (meditation). Hii ni nyenzo muhimu sana ya kukabiliana na changamoto kama vile msongo wa mawazo, kukata tamaa, kusikia uchungu, kuwa na hasira, wasiwasi, na hisia kama hizo.
Ili uweze kuimudu kozi hii na iwe na faida kwako ni muhimu kutokosa hata somo moja ambalo litakuijia kuanzia Novemba Mosi kwa wiki nane mfululizo.
Kila somo litaambatana na video yenye maelezo rahisi kwa lugha ya Kiswahili.
Karibu sana, na ikikupendeza, mkaribishe na mwenzio